2 Mambo ya Nyakati 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Mambo ya Nyakati 12 (Swahili) 2nd Chronicles 12 (English)

Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha torati ya Bwana, na Israeli wote pamoja naye. 2 Mambo ya Nyakati 12:1

It happened, when the kingdom of Rehoboam was established, and he was strong, that he forsook the law of Yahweh, and all Israel with him.

Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi Bwana; 2 Mambo ya Nyakati 12:2

It happened in the fifth year of king Rehoboam, that Shishak king of Egypt came up against Jerusalem, because they had trespassed against Yahweh,

mwenye magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi sitini elfu; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi. 2 Mambo ya Nyakati 12:3

with twelve hundred chariots, and sixty thousand horsemen. The people were without number who came with him out of Egypt: the Lubim, the Sukkiim, and the Ethiopians.

Akaitwaa miji yenye maboma iliyokuwa ya Yuda, akaja Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati 12:4

He took the fortified cities which pertained to Judah, and came to Jerusalem.

Ndipo akaja Shemaya nabii kwa Rehoboamu, na kwa wakuu wa Yuda, waliokusanyika Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki, akawaambia, Bwana asema hivi, Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki. 2 Mambo ya Nyakati 12:5

Now Shemaiah the prophet came to Rehoboam, and to the princes of Judah, who were gathered together to Jerusalem because of Shishak, and said to them, Thus says Yahweh, You have forsaken me, therefore have I also left you in the hand of Shishak.

Ndipo wakajinyenyekeza wakuu wa Israeli na mfalme; wakasema, Bwana ndiye mwenye haki. 2 Mambo ya Nyakati 12:6

Then the princes of Israel and the king humbled themselves; and they said, Yahweh is righteous.

Naye Bwana alipoona ya kwamba wamejinyenyekeza, neno la Bwana likamjia Shemaya, kusema, Wamejinyenyekeza; sitawaharibu; lakini nitawapa wokovu punde, wala ghadhabu yangu haitamwagika juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki. 2 Mambo ya Nyakati 12:7

When Yahweh saw that they humbled themselves, the word of Yahweh came to Shemaiah, saying, They have humbled themselves: I will not destroy them; but I will grant them some deliverance, and my wrath shall not be poured out on Jerusalem by the hand of Shishak.

Walakini watamtumikia; ili wapate kujua utumwa wangu, na huo utumwa wa falme za nchi. 2 Mambo ya Nyakati 12:8

Nevertheless they shall be his servants, that they may know my service, and the service of the kingdoms of the countries.

Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akapanda juu ya Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani. 2 Mambo ya Nyakati 12:9

So Shishak king of Egypt came up against Jerusalem, and took away the treasures of the house of Yahweh, and the treasures of the king's house: he took all away: he took away also the shields of gold which Solomon had made.

Mfalme Rehoboamu akafanya ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme. 2 Mambo ya Nyakati 12:10

King Rehoboam made in their place shields of brass, and committed them to the hands of the captains of the guard, who kept the door of the king's house.

Ikawa kila wakati mfalme alipoingia nyumbani mwa Bwana, wakaja walinzi wakazichukua, wakazirudisha tena chumbani mwa walinzi. 2 Mambo ya Nyakati 12:11

It was so, that as often as the king entered into the house of Yahweh, the guard came and bore them, and brought them back into the guard-chamber.

Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya Bwana ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekana katika Yuda mambo mema. 2 Mambo ya Nyakati 12:12

When he humbled himself, the wrath of Yahweh turned from him, so as not to destroy him altogether: and moreover in Judah there were good things [found].

Basi mfalme Rehoboamu akajitia nguvu katika Yerusalemu, akatawala; maana Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji aliouchagua Bwana miongoni mwa kabila zote za Israeli, ili aliweke huko jina lake. Na jina la mamaye aliitwa Naama Mwamoni. 2 Mambo ya Nyakati 12:13

So king Rehoboam strengthened himself in Jerusalem, and reigned: for Rehoboam was forty-one years old when he began to reign, and he reigned seventeen years in Jerusalem, the city which Yahweh had chosen out of all the tribes of Israel, to put his name there: and his mother's name was Naamah the Ammonitess.

Naye akatenda yaliyo maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute Bwana. 2 Mambo ya Nyakati 12:14

He did that which was evil, because he didn't set his heart to seek Yahweh.

Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza na ya mwisho, je! Hayakuandikwa katika tarehe za Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote. 2 Mambo ya Nyakati 12:15

Now the acts of Rehoboam, first and last, aren't they written in the histories of Shemaiah the prophet and of Iddo the seer, after the manner of genealogies? There were wars between Rehoboam and Jeroboam continually.

Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi. Na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.

2 Mambo ya Nyakati 12:16

Rehoboam slept with his fathers, and was buried in the city of David: and Abijah his son reigned in his place.