1 Mambo ya Nyakati 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 6 (Swahili) 1st Chronicles 6 (English)

Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. 1 Mambo ya Nyakati 6:1

The sons of Levi: Gershon, Kohath, and Merari.

Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. 1 Mambo ya Nyakati 6:2

The sons of Kohath: Amram, Izhar, and Hebron, and Uzziel.

Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 1 Mambo ya Nyakati 6:3

The children of Amram: Aaron, and Moses, and Miriam. The sons of Aaron: Nadab, and Abihu, Eleazar, and Ithamar.

Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua; 1 Mambo ya Nyakati 6:4

Eleazar became the father of Phinehas, Phinehas became the father of Abishua,

na Abishua akamzaa Buki; na Buki akamzaa Uzi; 1 Mambo ya Nyakati 6:5

and Abishua became the father of Bukki, and Bukki became the father of Uzzi,

na Uzi akamzaa Zerahia; na Zerahia akamzaa Merayothi, 1 Mambo ya Nyakati 6:6

and Uzzi became the father of Zerahiah, and Zerahiah became the father of Meraioth,

na Merayothi akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu; 1 Mambo ya Nyakati 6:7

Meraioth became the father of Amariah, and Amariah became the father of Ahitub,

na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Ahimaasi; 1 Mambo ya Nyakati 6:8

and Ahitub became the father of Zadok, and Zadok became the father of Ahimaaz,

na Ahimaasi akamzaa Azaria; na Azaria akamzaa Yohana; 1 Mambo ya Nyakati 6:9

and Ahimaaz became the father of Azariah, and Azariah became the father of Johanan,

na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu) 1 Mambo ya Nyakati 6:10

and Johanan became the father of Azariah, (he it is who executed the priest's office in the house that Solomon built in Jerusalem),

na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu; 1 Mambo ya Nyakati 6:11

and Azariah became the father of Amariah, and Amariah became the father of Ahitub,

na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu; 1 Mambo ya Nyakati 6:12

and Ahitub became the father of Zadok, and Zadok became the father of Shallum,

na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria; 1 Mambo ya Nyakati 6:13

and Shallum became the father of Hilkiah, and Hilkiah became the father of Azariah,

na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki; 1 Mambo ya Nyakati 6:14

and Azariah became the father of Seraiah, and Seraiah became the father of Jehozadak;

na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo Bwana alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza. 1 Mambo ya Nyakati 6:15

Jehozadak went [into captivity], when Yahweh carried away Judah and Jerusalem by the hand of Nebuchadnezzar.

Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. 1 Mambo ya Nyakati 6:16

The sons of Levi: Gershom, Kohath, and Merari.

Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei. 1 Mambo ya Nyakati 6:17

These are the names of the sons of Gershom: Libni and Shimei.

Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. 1 Mambo ya Nyakati 6:18

The sons of Kohath were Amram, and Izhar, and Hebron, and Uzziel.

Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao. 1 Mambo ya Nyakati 6:19

The sons of Merari: Mahli and Mushi. These are the families of the Levites according to their fathers' [houses].

Wa Gershoni; mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Yahathi, na mwanawe huyo ni Zima; 1 Mambo ya Nyakati 6:20

Of Gershom: Libni his son, Jahath his son, Zimmah his son,

na mwanawe huyo ni Yoa, na mwanawe huyo ni Ido, na mwanawe huyo ni Zera, na mwanawe huyo ni Yeatherai. 1 Mambo ya Nyakati 6:21

Joah his son, Iddo his son, Zerah his son, Jeatherai his son.

Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri; 1 Mambo ya Nyakati 6:22

The sons of Kohath: Amminadab his son, Korah his son, Assir his son,

na mwanawe huyo ni Elkana, na mwanawe huyo ni Ebiasafu, na mwanawe huyo ni Asiri; 1 Mambo ya Nyakati 6:23

Elkanah his son, and Ebiasaph his son, and Assir his son,

na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli. 1 Mambo ya Nyakati 6:24

Tahath his son, Uriel his son, Uzziah his son, and Shaul his son.

Na wana wa Elkana; Amasai, na Ahimothi. 1 Mambo ya Nyakati 6:25

The sons of Elkanah: Amasai, and Ahimoth.

Kwa habari za Elkana; wana wa Elkana; mwanawe huyo ni Sufu, na mwanawe huyo ni Tohu; 1 Mambo ya Nyakati 6:26

As for Elkanah, the sons of Elkanah: Zophai his son, and Nahath his son,

na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana. 1 Mambo ya Nyakati 6:27

Eliab his son, Jeroham his son, Elkanah his son.

Na wana wa Samweli; Yoeli, mzaliwa wa kwanza, na wa pili Abia. 1 Mambo ya Nyakati 6:28

The sons of Samuel: the firstborn [Joel], and the second Abijah.

Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza; 1 Mambo ya Nyakati 6:29

The sons of Merari: Mahli, Libni his son, Shimei his son, Uzzah his son,

na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya. 1 Mambo ya Nyakati 6:30

Shimea his son, Haggiah his son, Asaiah his son.

Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi juu ya kazi ya kuimba katika nyumba ya Bwana, sanduku lile lilipokwisha pata mahali pa kustarehe. 1 Mambo ya Nyakati 6:31

These are they whom David set over the service of song in the house of Yahweh, after that the ark had rest.

Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya Bwana huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao. 1 Mambo ya Nyakati 6:32

They ministered with song before the tent of the tent of meeting, until Solomon had built the house of Yahweh in Jerusalem: and they waited on their office according to their order.

Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli; 1 Mambo ya Nyakati 6:33

These are those who waited, and their sons. Of the sons of the Kohathites: Heman the singer, the son of Joel, the son of Samuel,

mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu; 1 Mambo ya Nyakati 6:34

the son of Elkanah, the son of Jeroham, the son of Eliel, the son of Toah,

mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai; 1 Mambo ya Nyakati 6:35

the son of Zuph, the son of Elkanah, the son of Mahath, the son of Amasai,

mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli; 1 Mambo ya Nyakati 6:36

the son of Elkanah, the son of Joel, the son of Azariah, the son of Zephaniah,

mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; 1 Mambo ya Nyakati 6:37

the son of Tahath, the son of Assir, the son of Ebiasaph, the son of Korah,

mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 6:38

the son of Izhar, the son of Kohath, the son of Levi, the son of Israel.

Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea; 1 Mambo ya Nyakati 6:39

His brother Asaph, who stood on his right hand, even Asaph the son of Berechiah, the son of Shimea,

mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya; 1 Mambo ya Nyakati 6:40

the son of Michael, the son of Baaseiah, the son of Malchijah,

mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido; 1 Mambo ya Nyakati 6:41

the son of Ethni, the son of Zerah, the son of Adaiah,

mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei; 1 Mambo ya Nyakati 6:42

the son of Ethan, the son of Zimmah, the son of Shimei,

mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi. 1 Mambo ya Nyakati 6:43

the son of Jahath, the son of Gershom, the son of Levi.

Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki; 1 Mambo ya Nyakati 6:44

On the left hand their brothers the sons of Merari: Ethan the son of Kishi, the son of Abdi, the son of Malluch,

mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia; 1 Mambo ya Nyakati 6:45

the son of Hashabiah, the son of Amaziah, the son of Hilkiah,

mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri; 1 Mambo ya Nyakati 6:46

the son of Amzi, the son of Bani, the son of Shemer,

mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi. 1 Mambo ya Nyakati 6:47

the son of Mahli, the son of Mushi, the son of Merari, the son of Levi.

Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 6:48

Their brothers the Levites were appointed for all the service of the tent of the house of God.

Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 6:49

But Aaron and his sons offered on the altar of burnt offering, and on the altar of incense, for all the work of the most holy place, and to make atonement for Israel, according to all that Moses the servant of God had commanded.

Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua; 1 Mambo ya Nyakati 6:50

These are the sons of Aaron: Eleazar his son, Phinehas his son, Abishua his son,

na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia; 1 Mambo ya Nyakati 6:51

Bukki his son, Uzzi his son, Zerahiah his son,

na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu; 1 Mambo ya Nyakati 6:52

Meraioth his son, Amariah his son, Ahitub his son,

na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi. 1 Mambo ya Nyakati 6:53

Zadok his son, Ahimaaz his son.

Basi haya ndiyo makao yao, sawasawa na marago yao mipakani mwao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza; 1 Mambo ya Nyakati 6:54

Now these are their dwelling-places according to their encampments in their borders: to the sons of Aaron, of the families of the Kohathites (for theirs was the [first] lot),

wakapewa Hebroni, katika nchi ya Yuda, na vijiji vyake vilivyouzunguka; 1 Mambo ya Nyakati 6:55

to them they gave Hebron in the land of Judah, and the suburbs of it round about it;

bali mashamba ya mji huo, na vijiji vyake, alipewa Kalebu, mwana wa Yefune. 1 Mambo ya Nyakati 6:56

but the fields of the city, and the villages of it, they gave to Caleb the son of Jephunneh.

Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:57

To the sons of Aaron they gave the cities of refuge, Hebron; Libnah also with its suburbs, and Jattir, and Eshtemoa with its suburbs,

na Holoni pamoja na viunga vyake, na Debiri pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:58

and Hilen with its suburbs, Debir with its suburbs,

na Ashani pamoja na viunga vyake, na Beth-shemeshi pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:59

and Ashan with its suburbs, and Beth-shemesh with its suburbs;

tena katika kabila ya Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu. 1 Mambo ya Nyakati 6:60

and out of the tribe of Benjamin, Geba with its suburbs, and Allemeth with its suburbs, and Anathoth with its suburbs. All their cities throughout their families were thirteen cities.

Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hiyo, yaani, nusu-kabila, nusu ya Manase. 1 Mambo ya Nyakati 6:61

To the rest of the sons of Kohath [were given] by lot, out of the family of the tribe, out of the half-tribe, the half of Manasseh, ten cities.

Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani. 1 Mambo ya Nyakati 6:62

To the sons of Gershom, according to their families, out of the tribe of Issachar, and out of the tribe of Asher, and out of the tribe of Naphtali, and out of the tribe of Manasseh in Bashan, thirteen cities.

Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Reubeni, na katika kabila ya Gadi, na katika kabila ya Zabuloni. 1 Mambo ya Nyakati 6:63

To the sons of Merari [were given] by lot, according to their families, out of the tribe of Reuben, and out of the tribe of Gad, and out of the tribe of Zebulun, twelve cities.

Na wana wa Israeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na viunga vyake. 1 Mambo ya Nyakati 6:64

The children of Israel gave to the Levites the cities with their suburbs.

Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila ya wana wa Yuda, na katika kabila ya wana wa Simeoni, na katika kabila ya wana wa Benyamini. 1 Mambo ya Nyakati 6:65

They gave by lot out of the tribe of the children of Judah, and out of the tribe of the children of Simeon, and out of the tribe of the children of Benjamin, these cities which are mentioned by name.

Na jamaa nyingine za wana wa Kohathi walikuwa na miji ya mipakani mwao katika kabila ya Efraimu. 1 Mambo ya Nyakati 6:66

Some of the families of the sons of Kohath had cities of their borders out of the tribe of Ephraim.

Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:67

They gave to them the cities of refuge, Shechem in the hill-country of Ephraim with its suburbs; Gezer also with its suburbs,

na Yokmeamu pamoja na viunga vyake, na Beth-horoni pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:68

and Jokmeam with its suburbs, and Beth Horon with its suburbs,

na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:69

and Aijalon with its suburbs, and Gath-rimmon with its suburbs;

na katika nusu-kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi. 1 Mambo ya Nyakati 6:70

and out of the half-tribe of Manasseh, Aner with its suburbs, and Bileam with its suburbs, for the rest of the family of the sons of Kohath.

Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:71

To the sons of Gershom [were given], out of the family of the half-tribe of Manasseh, Golan in Bashan with its suburbs, and Ashtaroth with its suburbs;

na katika kabila ya Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:72

and out of the tribe of Issachar, Kedesh with its suburbs, Daberath with its suburbs,

na Remethi pamoja na viunga vyake, na En-gaminu pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:73

and Ramoth with its suburbs, and Anem with its suburbs;

na katika kabila ya Asheri; Mishali pamoja na viunga vyake, na Abdoni pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:74

and out of the tribe of Asher, Mashal with its suburbs, and Abdon with its suburbs,

na Helkathi pamoja na viunga vyake, na Rehobu pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:75

and Hukok with its suburbs, and Rehob with its suburbs;

na katika kabila ya Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake. 1 Mambo ya Nyakati 6:76

and out of the tribe of Naphtali, Kedesh in Galilee with its suburbs, and Hammon with its suburbs, and Kiriathaim with its suburbs.

Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila ya Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:77

To the rest of [the Levites], the sons of Merari, [were given], out of the tribe of Zebulun, Rimmono with its suburbs, Tabor with its suburbs;

na ng'ambo ya mto wa Yordani huko Yeriko, upande wa mashariki wa Yordani, katika kabila ya Reubeni; Bezeri katika nyika pamoja na viunga vyake, na Yahasa pamoja na viunga vyake, 1 Mambo ya Nyakati 6:78

and beyond the Jordan at Jericho, on the east side of the Jordan, [were given them], out of the tribe of Reuben, Bezer in the wilderness with its suburbs, and Jahzah with its suburbs,

na Kedemothi pamoja na viunga vyake, na Mefaathi pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:79

and Kedemoth with its suburbs, and Mephaath with its suburbs;

na katika kabila ya Gadi; Ramothi katika Gileadi pamoja na viunga vyake, na Mahanaimu pamoja na viunga vyake; 1 Mambo ya Nyakati 6:80

and out of the tribe of Gad, Ramoth in Gilead with its suburbs, and Mahanaim with its suburbs,

na Heshboni pamoja na viunga vyake, na Yazeri pamoja na viunga vyake. 1 Mambo ya Nyakati 6:81

and Heshbon with its suburbs, and Jazer with its suburbs.