1 Mambo ya Nyakati 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 5 (Swahili) 1st Chronicles 5 (English)

Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza. 1 Mambo ya Nyakati 5:1

The sons of Reuben the firstborn of Israel (for he was the firstborn; but, because he defiled his father's couch, his birthright was given to the sons of Joseph the son of Israel; and the genealogy is not to be reckoned after the birthright.

Kwani Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; bali haki ile ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu); 1 Mambo ya Nyakati 5:2

For Judah prevailed above his brothers, and of him came the prince; but the birthright was Joseph's:)

wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi. 1 Mambo ya Nyakati 5:3

the sons of Reuben the firstborn of Israel: Hanoch, and Pallu, Hezron, and Carmi.

Wana wa Yoeli; mwanawe huyo ni Shemaya, na mwanawe huyo ni Gogu, na mwanawe huyo ni Shimei; 1 Mambo ya Nyakati 5:4

The sons of Joel: Shemaiah his son, Gog his son, Shimei his son,

na mwanawe huyo ni Mika, na mwanawe huyo ni Reaya, na mwanawe huyo ni Baali; 1 Mambo ya Nyakati 5:5

Micah his son, Reaiah his son, Baal his son,

na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni. 1 Mambo ya Nyakati 5:6

Beerah his son, whom Tilgath Pilneser king of Assyria carried away captive: he was prince of the Reubenites.

Na nduguze kwa jamaa zao, hapo ilipohesabiwa nasaba ya vizazi vyao; mkuu wao, Yeieli, na Zekaria, 1 Mambo ya Nyakati 5:7

His brothers by their families, when the genealogy of their generations was reckoned: the chief, Jeiel, and Zechariah,

na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hata kufika Nebo na Baal-meoni; 1 Mambo ya Nyakati 5:8

and Bela the son of Azaz, the son of Shema, the son of Joel, who lived in Aroer, even to Nebo and Baal Meon:

na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng'ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi. 1 Mambo ya Nyakati 5:9

and eastward he lived even to the entrance of the wilderness from the river Euphrates, because their cattle were multiplied in the land of Gilead.

Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi. 1 Mambo ya Nyakati 5:10

In the days of Saul, they made war with the Hagrites, who fell by their hand; and they lived in their tents throughout all the [land] east of Gilead.

Na wana wa Gadi walikuwa wakikaa kwa kuwaelekea, katika nchi ya Bashani mpaka Saleka; 1 Mambo ya Nyakati 5:11

The sons of Gad lived over against them, in the land of Bashan to Salecah:

Yoeli, alikuwa mkuu wao, na wa pili Shafamu, na Yanai, na Shafati, katika Bashani; 1 Mambo ya Nyakati 5:12

Joel the chief, and Shapham the second, and Janai, and Shaphat in Bashan.

na ndugu zao wa mbari za baba zao; Mikaeli, na Meshulamu, na Sheba, na Yorai, na Yakani, na Zia, na Eberi, watu saba. 1 Mambo ya Nyakati 5:13

Their brothers of their fathers' houses: Michael, and Meshullam, and Sheba, and Jorai, and Jacan, and Zia, and Eber, seven.

Hao ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yehishai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi; 1 Mambo ya Nyakati 5:14

These were the sons of Abihail, the son of Huri, the son of Jaroah, the son of Gilead, the son of Michael, the son of Jeshishai, the son of Jahdo, the son of Buz;

Ahi, mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa mkuu wa mbari za baba zao. 1 Mambo ya Nyakati 5:15

Ahi the son of Abdiel, the son of Guni, chief of their fathers' houses.

Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake. 1 Mambo ya Nyakati 5:16

They lived in Gilead in Bashan, and in its towns, and in all the suburbs of Sharon, as far as their borders.

Hao wote walihesabiwa kwa nasaba, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mfalme wa Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 5:17

All these were reckoned by genealogies in the days of Jotham king of Judah, and in the days of Jeroboam king of Israel.

Wana wa Reubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Manase, watu mashujaa, wawezao kuchukua ngao na upanga, na kupiga upinde, wenye ustadi katika kupigana vita, walikuwa watu arobaini na nne elfu mia saba na sitini, walioweza kwenda vitani. 1 Mambo ya Nyakati 5:18

The sons of Reuben, and the Gadites, and the half-tribe of Manasseh, of valiant men, men able to bear buckler and sword, and to shoot with bow, and skillful in war, were forty-four thousand seven hundred and sixty, that were able to go forth to war.

Nao wakapigana vita na Wahajiri; na Yeturi, na Nafishi, na Nodabu. 1 Mambo ya Nyakati 5:19

They made war with the Hagrites, with Jetur, and Naphish, and Nodab.

Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye. 1 Mambo ya Nyakati 5:20

They were helped against them, and the Hagrites were delivered into their hand, and all who were with them; for they cried to God in the battle, and he was entreated of them, because they put their trust in him.

Wakateka nyara ng'ombe zao, na ngamia zao hamsini elfu, na kondoo zao mia mbili na hamsini elfu, na punda zao elfu mbili; na watu mia elfu. 1 Mambo ya Nyakati 5:21

They took away their cattle; of their camels fifty thousand, and of sheep two hundred fifty thousand, and of donkeys two thousand, and of men one hundred thousand.

Kwani wengi walianguka waliouawa, kwa sababu vita vile vilikuwa vya Mungu. Nao wakakaa badala yao hata wakati wa ule uhamisho. 1 Mambo ya Nyakati 5:22

For there fell many slain, because the war was of God. They lived in their place until the captivity.

Na wana wa nusu-kabila ya Manase walikaa katika nchi; nao wakaongezeka kutoka Bashani mpaka Baal-hermoni, na Seniri, na mlima Hermoni. 1 Mambo ya Nyakati 5:23

The children of the half-tribe of Manasseh lived in the land: they increased from Bashan to Baal Hermon and Senir and Mount Hermon.

Na hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao; Eferi, na Ishi, na Elieli, na Azrieli, na Yeremia, na Hodavia, na Yadieli; watu hodari wa vita, watu mashuhuri, wakuu wa mbari za baba zao. 1 Mambo ya Nyakati 5:24

These were the heads of their fathers' houses: even Epher, and Ishi, and Eliel, and Azriel, and Jeremiah, and Hodaviah, and Jahdiel, mighty men of valor, famous men, heads of their fathers' houses.

Nao wakamwasi Mungu wa baba zao, wakaenda kufanya uasherati na miungu ya watu wa nchi, ambao Mungu alikuwa amewaangamiza mbele yao. 1 Mambo ya Nyakati 5:25

They trespassed against the God of their fathers, and played the prostitute after the gods of the peoples of the land, whom God destroyed before them.

Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru na roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo. 1 Mambo ya Nyakati 5:26

The God of Israel stirred up the spirit of Pul king of Assyria, and the spirit of Tilgath Pilneser king of Assyria, and he carried them away, even the Reubenites, and the Gadites, and the half-tribe of Manasseh, and brought them to Halah, and Habor, and Hara, and to the river of Gozan, to this day.