1 Mambo ya Nyakati 29 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 29 (Swahili) 1st Chronicles 29 (English)

Kisha mfalme Daudi akawaambia kusanyiko lote, Sulemani mwanangu, ambaye Mungu amemchagua peke yake, akali ni mchanga bado na mwororo, nayo kazi hii ni kubwa; kwani nyumba hii ya enzi si kwa mwanadamu, ila kwa Bwana, Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 29:1

David the king said to all the assembly, Solomon my son, whom alone God has chosen, is yet young and tender, and the work is great; for the palace is not for man, but for Yahweh God.

Basi kwa uwezo wangu wote nimeiwekea akiba nyumba ya Mungu wangu, dhahabu kwa vitu vya dhahabu, na fedha kwa vitu vya fedha, na shaba kwa vitu vya shaba, na chuma kwa vitu vya chuma, na miti kwa vitu vya miti; vito vya shohamu, na vya kujazia, vito vya njumu, na vya rangi mbalimbali, na mawe ya thamani ya kila namna, na marimari tele. 1 Mambo ya Nyakati 29:2

Now I have prepared with all my might for the house of my God the gold for the [things of] gold, and the silver for the [things of] silver, and the brass for the [things of] brass, the iron for the [things of] iron, and wood for the [things of] wood; onyx stones, and [stones] to be set, stones for inlaid work, and of various colors, and all manner of precious stones, and marble stones in abundance.

Nami tena kwa kuwa nimeiwekea nyumba ya Mungu wangu shauku yangu, nami ninayo hazina yangu mwenyewe ya dhahabu na fedha, naitoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, zaidi ya hiyo akiba niliyoiwekea tayari nyumba takatifu; 1 Mambo ya Nyakati 29:3

In addition, because I have set my affection on the house of my God, seeing that I have a treasure of my own of gold and silver, I give it to the house of my God, over and above all that I have prepared for the holy house,

yaani, talanta elfu tatu za dhahabu, za dhahabu ya Ofiri, na talanta elfu saba za fedha iliyosafika, ya kuzifunikiza kuta za nyumba; 1 Mambo ya Nyakati 29:4

even three thousand talents of gold, of the gold of Ophir, and seven thousand talents of refined silver, with which to overlay the walls of the houses;

ya dhahabu, kwa vitu vya dhahabu, na ya fedha kwa vitu vya fedha, na kwa kazi za kila namna zitakazofanywa kwa mikono ya mafundi. Ni nani basi ajitoaye kwa moyo ili ajiweke wakfu leo kwa Bwana? 1 Mambo ya Nyakati 29:5

of gold for the [things of] gold, and of silver for the [things of] silver, and for all manner of work [to be made] by the hands of artificers. Who then offers willingly to consecrate himself this day to Yahweh?

Ndipo wakuu wa mbari za mababa, na wakuu wa kabila za Israeli, na maakida wa maelfu na wa mamia, pamoja na wasimamizi wa kazi ya mfalme, wakajitoa kwa hiari yao; 1 Mambo ya Nyakati 29:6

Then the princes of the fathers' [houses], and the princes of the tribes of Israel, and the captains of thousands and of hundreds, with the rulers over the king's work, offered willingly;

nao wakatoa, kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu, dhahabu talanta elfu tano, na darkoni elfu kumi,na fedha taranta elfu kumi, na shaba taranta elfu kumi na nane ,na chuma taranta elfu mia. 1 Mambo ya Nyakati 29:7

and they gave for the service of the house of God of gold five thousand talents and ten thousand darics, and of silver ten thousand talents, and of brass eighteen thousand talents, and of iron a hundred thousand talents.

Na wale walioonekana kuwa na vito vya thamani wakavitoa vitiwe katika hazina ya nyumba ya Bwana, chini ya mkono wa Yehieli, Mgershoni. 1 Mambo ya Nyakati 29:8

They with whom [precious] stones were found gave them to the treasure of the house of Yahweh, under the hand of Jehiel the Gershonite.

Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu. 1 Mambo ya Nyakati 29:9

Then the people rejoiced, because they offered willingly, because with a perfect heart they offered willingly to Yahweh: and David the king also rejoiced with great joy.

Kwa hiyo Daudi akamhimidi Bwana, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele. 1 Mambo ya Nyakati 29:10

Therefore David blessed Yahweh before all the assembly; and David said, You are blessed, Yahweh, the God of Israel our father, forever and ever.

Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. 1 Mambo ya Nyakati 29:11

Yours, Yahweh, is the greatness, the power, the glory, the victory, and the majesty: for all that is in the heavens and in the earth is yours. Yours is the kingdom, Yahweh, and you are exalted as head above all.

Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote. 1 Mambo ya Nyakati 29:12

Both riches and honor come of you, and you rule over all; and in your hand is power and might; and it is in your hand to make great, and to give strength to all.

Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu. 1 Mambo ya Nyakati 29:13

Now therefore, our God, we thank you, and praise your glorious name.

Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea. 1 Mambo ya Nyakati 29:14

But who am I, and what is my people, that we should be able to offer so willingly as this? For all things come of you, and of your own have we given you.

Kwani sisi tu wageni mbele zako, na wasafiri, kama walivyokuwa baba zetu wote; ni kama kivuli siku zetu duniani, wala taraji ya kukaa hapana. 1 Mambo ya Nyakati 29:15

For we are strangers before you, and foreigners, as all our fathers were: our days on the earth are as a shadow, and there is no abiding.

Ee Bwana, Mungu wetu, akiba hii yote tuliyoiweka, ili tukujengee nyumba kwa ajili ya jina lako takatifu, yatoka yote mkononi mwako, na yote ni yako wewe. 1 Mambo ya Nyakati 29:16

Yahweh our God, all this store that we have prepared to build you a house for your holy name comes of your hand, and is all your own.

Nami najua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao. 1 Mambo ya Nyakati 29:17

I know also, my God, that you try the heart, and have pleasure in uprightness. As for me, in the uprightness of my heart I have willingly offered all these things: and now have I seen with joy your people, that are present here, offer willingly to you.

Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, baba zetu, ulilinde jambo hili milele katika fikira za mawazo ya mioyo ya watu wako, ukaiongoze mioyo yao kwako; 1 Mambo ya Nyakati 29:18

Yahweh, the God of Abraham, of Isaac, and of Israel, our fathers, keep this forever in the imagination of the thoughts of the heart of your people, and prepare their heart to you;

naye Sulemani mwanangu, umpe moyo mkamilifu, ili azishike amri zako, na shuhuda zako, na maagizo yako, akayatende hayo yote na kuijenga nyumba hii ya enzi, niliyoiwekea akiba. 1 Mambo ya Nyakati 29:19

and give to Solomon my son a perfect heart, to keep your commandments, your testimonies, and your statutes, and to do all these things, and to build the palace, for which I have made provision.

Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, Haya, mhimidini Bwana, Mungu wenu. Basi kusanyiko lote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao, wakainama vichwa vyao, wakamsujudia Bwana, na mfalme naye. 1 Mambo ya Nyakati 29:20

David said to all the assembly, Now bless Yahweh your God. All the assembly blessed Yahweh, the God of their fathers, and bowed down their heads, and worshiped Yahweh, and the king.

Wakamtolea Bwana dhabihu, wakamchinjia Bwana sadaka za kuteketezwa, siku ya pili yake, yaani, ng'ombe elfu, na kondoo waume elfu, na wana-kondoo elfu, pamoja na sadaka zao za vinywaji, na dhabihu nyingi kwa ajili ya Israeli wote; 1 Mambo ya Nyakati 29:21

They sacrificed sacrifices to Yahweh, and offered burnt offerings to Yahweh, on the next day after that day, even one thousand bulls, one thousand rams, and one thousand lambs, with their drink-offerings, and sacrifices in abundance for all Israel,

wakala na kunywa mbele za Bwana siku ile, kwa furaha kuu. Wakamtawaza Sulemani, mwana wa Daudi, mara ya pili, wakamtia mafuta mbele za Bwana, awe mkuu, na Sadoki awe kuhani. 1 Mambo ya Nyakati 29:22

and ate and drink before Yahweh on that day with great gladness. They made Solomon the son of David king the second time, and anointed him to Yahweh to be prince, and Zadok to be priest.

Ndipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Bwana, awe mfalme badala ya Daudi babaye, akafanikiwa; nao Israeli wote wakamtii. 1 Mambo ya Nyakati 29:23

Then Solomon sat on the throne of Yahweh as king instead of David his father, and prospered; and all Israel obeyed him.

Nao wakuu wote, na mashujaa, na wana wote wa mfalme Daudi nao, wakajitia chini ya mfalme Sulemani. 1 Mambo ya Nyakati 29:24

All the princes, the mighty men, and also all of the sons of king David submitted themselves to Solomon the king.

Naye Bwana akamtukuza Sulemani mno machoni pa Israeli wote, akampa fahari ya kifalme ya kumpita mfalme awaye yote aliyekuwa kabla yake katika Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 29:25

Yahweh magnified Solomon exceedingly in the sight of all Israel, and bestowed on him such royal majesty as had not been on any king before him in Israel.

Basi Daudi, mwana wa Yese, akawa mfalme juu ya Israeli wote. 1 Mambo ya Nyakati 29:26

Now David the son of Jesse reigned over all Israel.

Na wakati aliotawala juu ya Israeli, ulikuwa miaka arobaini; miaka saba alitawala Hebroni, na miaka thelathini na mitatu akatawala Yerusalemu. 1 Mambo ya Nyakati 29:27

The time that he reigned over Israel was forty years; he reigned seven years in Hebron, and thirty-three [years] reigned he in Jerusalem.

Akafa mwenye umri mwema, ameshiba siku, na mali, na heshima; naye Sulemani mwanawe akamiliki badala yake. 1 Mambo ya Nyakati 29:28

He died in a good old age, full of days, riches, and honor: and Solomon his son reigned in his place.

Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji; 1 Mambo ya Nyakati 29:29

Now the acts of David the king, first and last, behold, they are written in the history of Samuel the seer, and in the history of Nathan the prophet, and in the history of Gad the seer,

pamoja na kutawala kwake kote na nguvu zake, nazo zamani zilizompata yeye, na Israeli, na falme zote za nchi. 1 Mambo ya Nyakati 29:30

with all his reign and his might, and the times that went over him, and over Israel, and over all the kingdoms of the countries.