1 Mambo ya Nyakati 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 21 (Swahili) 1st Chronicles 21 (English)

Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 21:1

Satan stood up against Israel, and moved David to number Israel.

Basi Daudi akamwambia Yoabu, na wakuu wa watu, Nendeni kawahesabu Israeli toka Beer-sheba mpaka Dani; mkanipashe habari, nipate kujua jumla yao. 1 Mambo ya Nyakati 21:2

David said to Joab and to the princes of the people, Go, number Israel from Beersheba even to Dan; and bring me word, that I may know the sum of them.

Naye Yoabu akasema, Bwana na awaongeze watu wake mara mia hesabu yao ilivyo; lakini, bwana wangu mfalme, si wote watumishi wa bwana wangu? Mbona basi bwana wangu analitaka neno hili? Mbona awe sababu ya hatia kwa Israeli? 1 Mambo ya Nyakati 21:3

Joab said, Yahweh make his people a hundred times as many as they are: but, my lord the king, aren't they all my lord's servants? why does my lord require this thing? why will he be a cause of guilt to Israel?

Lakini neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu. Kwa hiyo Yoabu akaenda zake, akapita kati ya Israeli wote, akafika Yerusalemu. 1 Mambo ya Nyakati 21:4

Nevertheless the king's word prevailed against Joab. Therefore Joab departed, and went throughout all Israel, and came to Jerusalem.

Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu mia nne na sabini elfu, wenye kufuta panga. 1 Mambo ya Nyakati 21:5

Joab gave up the sum of the numbering of the people to David. All those of Israel were one million one hundred thousand men who drew sword: and in Judah were four hundred seventy thousand men who drew sword.

Lakini Lawi na Benyamini hakuwahesabu miongoni mwao; kwa sababu neno la mfalme limemchukiza Yoabu. 1 Mambo ya Nyakati 21:6

But he didn't count Levi and Benjamin among them; for the king's word was abominable to Joab.

Neno hilo likawa baya machoni pa Mungu; kwa hiyo akawapiga Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 21:7

God was displeased with this thing; therefore he struck Israel.

Naye Daudi akamwambia Mungu, Nimekosa sana, kwa kuwa nimelifanya jambo hili; lakini sasa uuondolee mbali, nakusihi, uovu wa mtumwa wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa. 1 Mambo ya Nyakati 21:8

David said to God, I have sinned greatly, in that I have done this thing: but now, put away, I beg you, the iniquity of your servant; for I have done very foolishly.

Naye Bwana akanena na Gadi, mwonaji wake Daudi, akisema, 1 Mambo ya Nyakati 21:9

Yahweh spoke to Gad, David's seer, saying,

Nenda ukanene na Daudi, ukisema, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya ujichagulie moja, nikutendee hilo. 1 Mambo ya Nyakati 21:10

Go and speak to David, saying, Thus says Yahweh, I offer you three things: choose you one of them, that I may do it to you.

Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo; 1 Mambo ya Nyakati 21:11

So Gad came to David, and said to him, Thus says Yahweh, Take which you will:

miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma. 1 Mambo ya Nyakati 21:12

either three years of famine; or three months to be consumed before your foes, while the sword of your enemies overtakes you; or else three days the sword of Yahweh, even pestilence in the land, and the angel of Yahweh destroying throughout all the borders of Israel. Now therefore consider what answer I shall return to him who sent me.

Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu. 1 Mambo ya Nyakati 21:13

David said to Gad, I am in a great strait: let me fall, I pray, into the hand of Yahweh; for very great are his mercies: and let me not fall into the hand of man.

Basi Bwana akawaletea Israeli tauni; nao wakaanguka wa Israeli watu sabini elfu. 1 Mambo ya Nyakati 21:14

So Yahweh sent a pestilence on Israel; and there fell of Israel seventy thousand men.

Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, Bwana akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa Bwana akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi. 1 Mambo ya Nyakati 21:15

God sent an angel to Jerusalem to destroy it: and as he was about to destroy, Yahweh saw, and he repented him of the evil, and said to the destroying angel, It is enough; now stay your hand. The angel of Yahweh was standing by the threshing floor of Ornan the Jebusite.

Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa Bwana amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusakmu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifulifuli, nao wamevaa nguo za magunia. 1 Mambo ya Nyakati 21:16

David lifted up his eyes, and saw the angel of Yahweh standing between earth and the sky, having a drawn sword in his hand stretched out over Jerusalem. Then David and the elders, clothed in sackcloth, fell on their faces.

Daudi akamwambia Mungu, Je! Si mimi niliyeamuru watu wahesabiwe? Naam, mimi ndimi niliyekosa, na kufanya yaliyo maovu sana; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako, nakusihi, Ee Bwana, Mungu wangu, na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya babangu; wala si juu ya watu wako, hata wao wapigwe. 1 Mambo ya Nyakati 21:17

David said to God, Isn't it I who commanded the people to be numbered? It is even I who have sinned and done very wickedly; but these sheep, what have they done? Please let your hand, O Yahweh my God, be against me, and against my father's house; but not against your people, that they should be plagued.

Ndipo huyo malaika wa Bwana akamwamuru Gadi kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie Bwana madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi. 1 Mambo ya Nyakati 21:18

Then the angel of Yahweh commanded Gad to tell David, that David should go up, and raise an altar to Yahweh in the threshing floor of Ornan the Jebusite.

Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, alilolinena kwa jina la Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 21:19

David went up at the saying of Gad, which he spoke in the name of Yahweh.

Arauna alipogeuka, na kumwona yule malaika, ndipo yeye na wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha. Naye Arauna alikuwa akipura ngano. 1 Mambo ya Nyakati 21:20

Ornan turned back, and saw the angel; and his four sons who were with him hid themselves. Now Ornan was threshing wheat.

Basi Daudi alipokuwa akimjia Arauna, Arauna akatazama, akamwona Daudi, akatoka katika kile kiwanja, akamsujudia Daudi kifulifuli hata nchi. 1 Mambo ya Nyakati 21:21

As David came to Ornan, Ornan looked and saw David, and went out of the threshing floor, and bowed himself to David with his face to the ground.

Ndipo Daudi akamwambia Arauna, Unipe mahali pa kiwanja hiki, ili kwamba nimjengee Bwana madhabahu hapa; kwa thamani yake kamili utanipa; ili kwamba tauni izuiliwe katika watu. 1 Mambo ya Nyakati 21:22

Then David said to Ornan, Give me the place of this threshing floor, that I may build thereon an altar to Yahweh: for the full price shall you give it me, that the plague may be stayed from the people.

Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng'ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa. 1 Mambo ya Nyakati 21:23

Ornan said to David, Take it to you, and let my lord the king do that which is good in his eyes: behold, I give [you] the oxen for burnt offerings, and the threshing instruments for wood, and the wheat for the meal-offering; I give it all.

Mfalme Daudi akamwambia Arauna, La, sivyo, lakini kweli nitazinunua kwa thamani yake kamili; kwani sitamtwalia Bwana kilicho chako, wala kutoa sadaka ya kuteketezwa isiyo na gharama. 1 Mambo ya Nyakati 21:24

King David said to Ornan, No; but I will most assuredly buy it for the full price: for I will not take that which is your for Yahweh, nor offer a burnt-offering without cost.

Basi Daudi akampimia Arauna thamani ya mahali pale shekeli mia sita za dhahabu kwa uzani 1 Mambo ya Nyakati 21:25

So David gave to Ornan for the place six hundred shekels of gold by weight.

Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana Bwana; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa. 1 Mambo ya Nyakati 21:26

David built there an altar to Yahweh, and offered burnt offerings and peace-offerings, and called on Yahweh; and he answered him from the sky by fire on the altar of burnt offering.

Bwana naye akamwamuru malaika; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena. 1 Mambo ya Nyakati 21:27

Yahweh commanded the angel; and he put up his sword again into the sheath of it.

Wakati huo, Daudi alipoona ya kwamba Bwana amemwitikia katika kiwanja cha Arauna, Myebusi, ndipo hutoa dhabihu huko. 1 Mambo ya Nyakati 21:28

At that time, when David saw that Yahweh had answered him in the threshing floor of Ornan the Jebusite, then he sacrificed there.

Kwa maana ile maskani ya Bwana, aliyoifanya Musa jangwani, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, vilikuwapo wakati huo mahali pa juu pa Gibeoni. 1 Mambo ya Nyakati 21:29

For the tent of Yahweh, which Moses made in the wilderness, and the altar of burnt offering, were at that time in the high place at Gibeon.

Wala Daudi hakuweza kwenda mbele yake ili kumwuliza Mungu; kwa sababu aliona hofu kwa ajili ya upanga wa yule malaika wa Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 21:30

But David couldn't go before it to inquire of God; for he was afraid because of the sword of the angel of Yahweh.