1 Mambo ya Nyakati 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 20 (Swahili) 1st Chronicles 20 (English)

Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza. 1 Mambo ya Nyakati 20:1

It happened, at the time of the return of the year, at the time when kings go out [to battle], that Joab led forth the army, and wasted the country of the children of Ammon, and came and besieged Rabbah. But David stayed at Jerusalem. Joab struck Rabbah, and overthrew it.

Kisha Daudi akamtwalia mfalme wao taji toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana. 1 Mambo ya Nyakati 20:2

David took the crown of their king from off his head, and found it to weigh a talent of gold, and there were precious stones in it; and it was set on David's head: and he brought forth the spoil of the city, exceeding much.

Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawakata-kata kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote. 1 Mambo ya Nyakati 20:3

He brought forth the people who were therein, and cut [them] with saws, and with harrows of iron, and with axes. Thus did David to all the cities of the children of Ammon. David and all the people returned to Jerusalem.

Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gobu; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai; nao wakashindwa. 1 Mambo ya Nyakati 20:4

It happened after this, that there arose war at Gezer with the Philistines: then Sibbecai the Hushathite killed Sippai, of the sons of the giant; and they were subdued.

Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti ,ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji. 1 Mambo ya Nyakati 20:5

There was again war with the Philistines; and Elhanan the son of Jair killed Lahmi the brother of Goliath the Gittite, the staff of whose spear was like a weaver's beam.

Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai. 1 Mambo ya Nyakati 20:6

There was again war at Gath, where was a man of great stature, whose fingers and toes were twenty-four, six [on each hand], and six [on each foot]; and he also was born to the giant.

Naye huyo alipowatukana Israeli, Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua. 1 Mambo ya Nyakati 20:7

When he defied Israel, Jonathan the son of Shimea David's brother killed him.

Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi,nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi , na kwa mkono wa watumishi wake.

1 Mambo ya Nyakati 20:8

These were born to the giant in Gath; and they fell by the hand of David, and by the hand of his servants.