1 Mambo ya Nyakati 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 19 (Swahili) 1st Chronicles 19 (English)

Ikawa baada ya hayo, Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, akafa, akamiliki mwanawe mahali pake. 1 Mambo ya Nyakati 19:1

It happened after this, that Nahash the king of the children of Ammon died, and his son reigned in his place.

Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahashi, kwa kuwa babaye alinitendea mimi wema. Basi Daudi akapeleka wajumbe ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni kwa Hanuni, ili wamtulize. 1 Mambo ya Nyakati 19:2

David said, I will show kindness to Hanun the son of Nahash, because his father shown kindness to me. So David sent messengers to comfort him concerning his father. David's servants came into the land of the children of Ammon to Hanun, to comfort him.

Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, Je! Waona Daudi amheshimu babayo kwa kukupelekea wafariji? Je! Hawakukujia watumishi wake ili kuiangalia nchi, na kuiangamiza, na kuipeleleza? 1 Mambo ya Nyakati 19:3

But the princes of the children of Ammon said to Hanun, Think you that David does honor your father, in that he has sent comforters to you? Aren't his servants come to you to search, and to overthrow, and to spy out the land?

Basi Hanuni akawatwaa watumishi wa Daudi, akawanyoa, akawakatia nguo zao katikati, hata matakoni, akawatoa waende zao. 1 Mambo ya Nyakati 19:4

So Hanun took David's servants, and shaved them, and cut off their garments in the middle, even to their buttocks, and sent them away.

Wakaenda watu wakamwambia Daudi jinsi walivyotendewa wale watu. Naye akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi. 1 Mambo ya Nyakati 19:5

Then there went certain persons, and told David how the men were served. He sent to meet them; for the men were greatly ashamed. The king said, Stay at Jericho until your beards be grown, and then return.

Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakapeleka talanta elfu za fedha ili kujiajiria magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba. 1 Mambo ya Nyakati 19:6

When the children of Ammon saw that they had made themselves odious to David, Hanun and the children of Ammon sent one thousand talents of silver to hire them chariots and horsemen out of Mesopotamia, and out of Arammaacah, and out of Zobah.

Basi wakajiajiria magari thelathini na mbili elfu, na mfalme wa Maaka na watu wake; nao walikuja wakatua mbele ya Medeba. Na wana wa Amoni wakakusanyika kutoka miji yao, wakaja vitani. 1 Mambo ya Nyakati 19:7

So they hired them thirty-two thousand chariots, and the king of Maacah and his people, who came and encamped before Medeba. The children of Ammon gathered themselves together from their cities, and came to battle.

Basi Daudi aliposikia habari akamtuma Yoabu, na jeshi lote la mashujaa. 1 Mambo ya Nyakati 19:8

When David heard of it, he sent Joab, and all the host of the mighty men.

Wakatoka wana wa Amoni, wakapanga vita langoni pa mji; na hao wafalme waliokuja walikuwa peke yao uwandani. 1 Mambo ya Nyakati 19:9

The children of Ammon came out, and put the battle in array at the gate of the city: and the kings who had come were by themselves in the field.

Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami. 1 Mambo ya Nyakati 19:10

Now when Joab saw that the battle was set against him before and behind, he chose of all the choice men of Israel, and put them in array against the Syrians.

Na hao watu waliosalia akawatia mikononi mwa Abishai, nduguye, nao wakajipanga juu ya wana wa Amoni. 1 Mambo ya Nyakati 19:11

The rest of the people he committed into the hand of Abishai his brother; and they put themselves in array against the children of Ammon.

Akasema, Wakiwa Washami ni hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia; lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakusaidia wewe. 1 Mambo ya Nyakati 19:12

He said, If the Syrians be too strong for me, then you shall help me; but if the children of Ammon be too strong for you, then I will help you.

Uwe hodari, tukajitie moyo mkuu kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye Bwana afanye yaliyo mema machoni pake. 1 Mambo ya Nyakati 19:13

Be of good courage, and let us play the man for our people, and for the cities of our God: and Yahweh do that which seems him good.

Basi Yoabu, na watu waliokuwa pamoja naye, wakakaribia kupigana na Washami; nao wakakimbia mbele yake. 1 Mambo ya Nyakati 19:14

So Joab and the people who were with him drew near before the Syrians to the battle; and they fled before him.

Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, nduguye, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akaja Yerusalemu. 1 Mambo ya Nyakati 19:15

When the children of Ammon saw that the Syrians were fled, they likewise fled before Abishai his brother, and entered into the city. Then Joab came to Jerusalem.

Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakapeleka wajumbe, wakawavuta Washami walioko ng'ambo ya Mto, na Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza. 1 Mambo ya Nyakati 19:16

When the Syrians saw that they were put to the worse before Israel, they sent messengers, and drew forth the Syrians who were beyond the River, with Shophach the captain of the host of Hadarezer at their head.

Alipoambiwa Daudi; akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye. 1 Mambo ya Nyakati 19:17

It was told David; and he gathered all Israel together, and passed over the Jordan, and came on them, and set the battle in array against them. So when David had put the battle in array against the Syrians, they fought with him.

Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari saba elfu, na askari waendao kwa miguu arobaini elfu, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi. 1 Mambo ya Nyakati 19:18

The Syrians fled before Israel; and David killed of the Syrians [the men of] seven thousand chariots, and forty thousand footmen, and killed Shophach the captain of the host.

Na watumwa wa Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Daudi, wakamtumikia; wala Washami hawakukubali kuwasaidia wana wa Amoni tena.

1 Mambo ya Nyakati 19:19

When the servants of Hadarezer saw that they were put to the worse before Israel, they made peace with David, and served him: neither would the Syrians help the children of Ammon any more.