1 Mambo ya Nyakati 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 13 (Swahili) 1st Chronicles 13 (English)

Kisha Daudi akafanya shauri na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, naam, na kila kiongozi. 1 Mambo ya Nyakati 13:1

David consulted with the captains of thousands and of hundreds, even with every leader.

Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa Bwana, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu; 1 Mambo ya Nyakati 13:2

David said to all the assembly of Israel, If it seem good to you, and if it be of Yahweh our God, let us send abroad everywhere to our brothers who are left in all the land of Israel, with whom the priests and Levites are in their cities that have suburbs, that they may gather themselves to us;

nasi tujirudishie tena sanduku la Mungu wetu; maana hamkuuliza neno kwa hilo katika siku za Sauli. 1 Mambo ya Nyakati 13:3

and let us bring again the ark of our God to us: for we didn't seek it in the days of Saul.

Nao jamii nzima wakasema ya kwamba watafanya hivyo; kwa kuwa neno hilo lilikuwa jema machoni pa watu wote. 1 Mambo ya Nyakati 13:4

All the assembly said that they would do so; for the thing was right in the eyes of all the people.

Basi Daudi akawakusanya Israeli wote, toka Shihori, kijito cha Misri, hata pa kuingilia Hamathi, ili kwamba walilete sanduku la Mungu kutoka Kiriath-yearimu. 1 Mambo ya Nyakati 13:5

So David assembled all Israel together, from the Shihor [the brook] of Egypt even to the entrance of Hamath, to bring the ark of God from Kiriath Jearim.

Basi Daudi akapanda, yeye na Israeli wote, mpaka Baala, ndio Kiriath-yearimu, ulio wa Yuda, ili kulileta toka huko sanduku la Mungu, Bwana akaaye juu ya makerubi, lililoitwa kwa Jina lake. 1 Mambo ya Nyakati 13:6

David went up, and all Israel, to Baalah, [that is], to Kiriath Jearim, which belonged to Judah, to bring up from there the ark of God Yahweh that sits [above] the cherubim, that is called by the Name.

Wakalipandisha sanduku la Mungu juu ya gari jipya kutoka nyumba ya Abinadabu; na Uza na Ahio wakaliendesha lile gari. 1 Mambo ya Nyakati 13:7

They carried the ark of God on a new cart, [and brought it] out of the house of Abinadab: and Uzza and Ahio drove the cart.

Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta. 1 Mambo ya Nyakati 13:8

David and all Israel played before God with all their might, even with songs, and with harps, and with psalteries, and with tambourines, and with cymbals, and with trumpets.

Hata walipofika penye uga wa Nakoni, Uza akaunyosha mkono wake alishike sanduku; kwa maana wale ng'ombe walikunguwaa. 1 Mambo ya Nyakati 13:9

When they came to the threshing floor of Chidon, Uzza put forth his hand to hold the ark; for the oxen stumbled.

Ndipo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hata akafa pale pale mbele za Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 13:10

The anger of Yahweh was kindled against Uzza, and he struck him, because he put forth his hand to the ark; and there he died before God.

Naye Daudi akaona uchungu, kwa kuwa Bwana amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo. 1 Mambo ya Nyakati 13:11

David was displeased, because Yahweh had broken forth on Uzza; and he called that place Perez Uzza, to this day.

Naye Daudi akamwogopa Mungu siku ile, akasema, Nitajileteaje sanduku la Mungu kwangu? 1 Mambo ya Nyakati 13:12

David was afraid of God that day, saying, How shall I bring the ark of God home to me?

Basi Daudi hakujichukulia sanduku mjini mwa Daudi, ila akalihamisha kando na kulitia nyumbani kwa Obed-edomu Mgiti. 1 Mambo ya Nyakati 13:13

So David didn't move the ark to him into the city of David, but carried it aside into the house of Obed-edom the Gittite.

Sanduku la Mungu likakaa na jamaa ya Obed-edomu, nyumbani mwake, muda wa miezi mitatu; naye Bwana akaibariki nyumba ya Obed-edomu, na yote aliyokuwa nayo. 1 Mambo ya Nyakati 13:14

The ark of God remained with the family of Obed-edom in his house three months: and Yahweh blessed the house of Obed-edom, and all that he had.