1 Mambo ya Nyakati 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 12 (Swahili) 1st Chronicles 12 (English)

Basi hawa ndio wale waliomjia Daudi huko Siklagi, alipokuwa akijificha kwa ajili ya Sauli, mwana wa Kishi; nao walikuwamo miongoni mwa wale mashujaa, waliomsaidia vitani. 1 Mambo ya Nyakati 12:1

Now these are those who came to David to Ziklag, while he yet kept himself close because of Saul the son of Kish; and they were among the mighty men, his helpers in war.

Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini. 1 Mambo ya Nyakati 12:2

They were armed with bows, and could use both the right hand and the left in slinging stones and in shooting arrows from the bow: they were of Saul's brothers of Benjamin.

Mkubwa wao alikuwa Ahiezeri, kisha Yoashi, wana wa Shemaa Mgibeathi; na Yezieli, na Peleti, wana wa Azmawethi; na Beraka, na Yehu Mwanathothi; 1 Mambo ya Nyakati 12:3

The chief was Ahiezer; then Joash, the sons of Shemaah the Gibeathite, and Jeziel, and Pelet, the sons of Azmaveth, and Beracah, and Jehu the Anathothite,

na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi; 1 Mambo ya Nyakati 12:4

and Ishmaiah the Gibeonite, a mighty man among the thirty, and over the thirty, and Jeremiah, and Jahaziel, and Johanan, and Jozabad the Gederathite,

Eluzai, na Yerimothi, na Bealia, na Shemaria, na Shefatia Mharufi; 1 Mambo ya Nyakati 12:5

Eluzai, and Jerimoth, and Bealiah, and Shemariah, and Shephatiah the Haruphite,

Elkana, na Ishia, na Azaleli, na Yoezeri, na Yashobeamu, Wakora; 1 Mambo ya Nyakati 12:6

Elkanah, and Isshiah, and Azarel, and Joezer, and Jashobeam, the Korahites,

na Yoela, na Zebadia, wana wa Yerohamu, wa Gedori. 1 Mambo ya Nyakati 12:7

and Joelah, and Zebadiah, the sons of Jeroham of Gedor.

Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima; 1 Mambo ya Nyakati 12:8

Of the Gadites there separated themselves to David to the stronghold in the wilderness, mighty men of valor, men trained for war, that could handle shield and spear; whose faces were like the faces of lions, and they were as swift as the roes on the mountains;

Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu; 1 Mambo ya Nyakati 12:9

Ezer the chief, Obadiah the second, Eliab the third,

Mishmana wa nne, Yeremia wa tano; 1 Mambo ya Nyakati 12:10

Mishmannah the fourth, Jeremiah the fifth,

Atai wa sita, Elieli wa saba; 1 Mambo ya Nyakati 12:11

Attai the sixth, Eliel the seventh,

Yohana wa nane, Elzabadi wa kenda; 1 Mambo ya Nyakati 12:12

Johanan the eighth, Elzabad the ninth,

Yeremia wa kumi, Makbanai wa kumi na moja. 1 Mambo ya Nyakati 12:13

Jeremiah the tenth, Machbannai the eleventh.

Hao wa wana wa Gadi walikuwa maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu. 1 Mambo ya Nyakati 12:14

These of the sons of Gad were captains of the host: he who was least was equal to one hundred, and the greatest to one thousand.

Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia. 1 Mambo ya Nyakati 12:15

These are those who went over the Jordan in the first month, when it had overflowed all its banks; and they put to flight all them of the valleys, both toward the east, and toward the west.

Tena wakafika ngomeni kwa Daudi baadhi ya wana wa Benyamini na Yuda. 1 Mambo ya Nyakati 12:16

There came of the children of Benjamin and Judah to the stronghold to David.

Naye Daudi akatoka ili kuwalaki, akajibu, akawaambia, Kama mmenijia kwa amani ili kunisaidia, basi moyo wangu utaambatana nanyi; lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu, kwa kuwa hamna udhalimu mikononi mwangu, Mungu wa baba zetu na alitazame neno hili, na kulikemea. 1 Mambo ya Nyakati 12:17

David went out to meet them, and answered them, If you be come peaceably to me to help me, my heart shall be knit to you; but if [you be come] to betray me to my adversaries, seeing there is no wrong in my hands, the God of our fathers look thereon, and rebuke it.

Ndipo roho ikamjilia Abishai, mkuu wa wale thelathini, naye akasema, Sisi tu watu wako, Ee Daudi; Na wa upande wako, Ee mwana wa Yese; Amani, naam, amani iwe kwako, Na amani iwe kwao wakusaidiao; Maana akusaidiye ndiye Mungu wako. Ndipo Daudi akawakaribisha, akawaweka wawe maakida wa kile kikosi. 1 Mambo ya Nyakati 12:18

Then the Spirit came on Amasai, who was chief of the thirty, [and he said], "We are yours, David, and on your side, you son of Jesse: peace, peace be to you, and peace be to your helpers; for your God helps you." Then David received them, and made them captains of the band.

Wa Manase pia wengine walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, kwa hatari ya vichwa vyetu atamwangukia bwana wake Sauli. 1 Mambo ya Nyakati 12:19

Of Manasseh also there fell away some to David, when he came with the Philistines against Saul to battle: but they didn't help them; for the lords of the Philistines sent him away after consultation, saying, He will fall away to his master Saul to the jeopardy of our heads.

Naye alipokuwa akienda Siklagi, wakamwangukia hawa wa Manase, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, maakida wa maelfu waliokuwa wa Manase. 1 Mambo ya Nyakati 12:20

As he went to Ziklag, there fell to him of Manasseh, Adnah, and Jozabad, and Jediael, and Michael, and Jozabad, and Elihu, and Zillethai, captains of thousands who were of Manasseh.

Wakamsaidia Daudi juu ya kile kikosi kilichomshambulia; kwani walikuwa waume mashujaa wote, nao wakawa maakida jeshini. 1 Mambo ya Nyakati 12:21

They helped David against the band of rovers: for they were all mighty men of valor, and were captains in the host.

Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 12:22

For from day to day men came to David to help him, until there was a great host, like the host of God.

Na hizi ni hesabu za vichwa vya watu wenye silaha za vita, waliokuja Hebroni kwa Daudi, ili kumgeuzia ufalme wa Sauli, sawasawa na neno la Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 12:23

These are the numbers of the heads of those who were armed for war, who came to David to Hebron, to turn the kingdom of Saul to him, according to the word of Yahweh.

Wana wa Yuda, waliochukua ngao na mkuki, walikuwa elfu sita na mia nane, wenye silaha za vita. 1 Mambo ya Nyakati 12:24

The children of Judah who bore shield and spear were six thousand and eight hundred, armed for war.

Wa wana wa Simeoni, waume mashujaa wa vita, elfu saba na mia moja. 1 Mambo ya Nyakati 12:25

Of the children of Simeon, mighty men of valor for the war, seven thousand and one hundred.

Wa wana wa Lawi, elfu nne na mia sita. 1 Mambo ya Nyakati 12:26

Of the children of Levi four thousand and six hundred.

Na Yehoyada alikuwa kichwa cha mbari ya Haruni, na pamoja naye walikuwa elfu tatu na mia saba; 1 Mambo ya Nyakati 12:27

Jehoiada was the leader of [the house of] Aaron; and with him were three thousand and seven hundred,

tena Sadoki, kijana shujaa, na wa nyumba ya babaye, maakida ishirini na wawili. 1 Mambo ya Nyakati 12:28

and Zadok, a young man mighty of valor, and of his father's house twenty-two captains.

Na wa wana wa Benyamini nduguze Sauli, elfu tatu; kwani hata sasa walio wengi wao walikuwa wameuhifadhi uaminifu wao kwa nyumba ya Sauli. 1 Mambo ya Nyakati 12:29

Of the children of Benjamin, the brothers of Saul, three thousand: for hitherto the greatest part of them had kept their allegiance to the house of Saul.

Na wa wana wa Efraimu, ishirini elfu na mia nane, waume mashujaa, watu wenye sifa katika mbari za baba zao. 1 Mambo ya Nyakati 12:30

Of the children of Ephraim twenty thousand eight hundred, mighty men of valor, famous men in their fathers' houses.

Na wa nusu kabila ya Manase, kumi na nane elfu, waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme. 1 Mambo ya Nyakati 12:31

Of the half-tribe of Manasseh eighteen thousand, who were mentioned by name, to come and make David king.

Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao. 1 Mambo ya Nyakati 12:32

Of the children of Issachar, men who had understanding of the times, to know what Israel ought to do, the heads of them were two hundred; and all their brothers were at their commandment.

Wa Zabuloni, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila namna, hamsini elfu; askari wastadi wasiokuwa wenye moyo wa kusita-sita. 1 Mambo ya Nyakati 12:33

Of Zebulun, such as were able to go out in the host, who could set the battle in array, with all manner of instruments of war, fifty thousand, and who could order [the battle array, and were] not of double heart.

Na wa Naftali, maakida elfu, na pamoja nao watu wenye ngao na mkuki thelathini na saba elfu. 1 Mambo ya Nyakati 12:34

Of Naphtali one thousand captains, and with them with shield and spear thirty-seven thousand.

Na wa Wadani, watu hodari wa kupanga vita, ishirini na nane elfu na mia sita. 1 Mambo ya Nyakati 12:35

Of the Danites who could set the battle in array, twenty-eight thousand six hundred.

Na wa Asheri, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, arobaini elfu. 1 Mambo ya Nyakati 12:36

Of Asher, such as were able to go out in the host, who could set the battle in array, forty thousand.

Tena, ng'ambo ya pili ya Yordani, wa Wareubeni, na wa Wagadi, na wa nusu kabila ya Manase, wenye zana za vita za kupigania za kila namna, mia na ishirini elfu. 1 Mambo ya Nyakati 12:37

On the other side of the Jordan, of the Reubenites, and the Gadites, and of the half-tribe of Manasseh, with all manner of instruments of war for the battle, one hundred twenty thousand.

Hao wote, watu wa vita, askari wastadi, wakaja Hebroni wenye moyo mkamilifu, ili kumtawaza Daudi awe mfalme juu ya Israeli wote; tena wote waliosalia wa Israeli nao walikuwa na moyo mmoja kwamba wamtawaze Daudi. 1 Mambo ya Nyakati 12:38

All these being men of war, who could order the battle array, came with a perfect heart to Hebron, to make David king over all Israel: and all the rest also of Israel were of one heart to make David king.

Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari. 1 Mambo ya Nyakati 12:39

They were there with David three days, eating and drinking; for their brothers had made preparation for them.

Zaidi ya hayo, wale waliokuwa karibu nao, hata mpaka kwa Isakari, na Zabuloni, na Naftali, wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng'ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng'ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 12:40

Moreover those who were near to them, [even] as far as Issachar and Zebulun and Naphtali, brought bread on donkeys, and on camels, and on mules, and on oxen, food of meal, cakes of figs, and clusters of raisins, and wine, and oil, and oxen, and sheep in abundance: for there was joy in Israel.