1 Mambo ya Nyakati 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 11 (Swahili) 1st Chronicles 11 (English)

Ndipo Israeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako. 1 Mambo ya Nyakati 11:1

Then all Israel gathered themselves to David to Hebron, saying, Behold, we are your bone and your flesh.

Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye Bwana, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 11:2

In times past, even when Saul was king, it was you who led out and brought in Israel: and Yahweh your God said to you, You shall be shepherd of my people Israel, and you shall be prince over my people Israel.

Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za Bwana; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la Bwana kwa mkono wa Samweli. 1 Mambo ya Nyakati 11:3

So all the elders of Israel came to the king to Hebron; and David made a covenant with them in Hebron before Yahweh; and they anointed David king over Israel, according to the word of Yahweh by Samuel.

Kisha Daudi na Israeli wote wakaenda Yerusalemu, (ndio Yebusi;) nao Wayebusi, wenyeji wa nchi, walikuwamo. 1 Mambo ya Nyakati 11:4

David and all Israel went to Jerusalem (the same is Jebus); and the Jebusites, the inhabitants of the land, were there.

Na hao wenyeji wa Yebusi wakamwambia Daudi, Hutaingia humu. Walakini Daudi akaitwaa ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi. 1 Mambo ya Nyakati 11:5

The inhabitants of Jebus said to David, You shall not come in here. Nevertheless David took the stronghold of Zion; the same is the city of David.

Naye Daudi akasema, Mtu ye yote atakayekuwa wa kwanza wa kuwapiga Wayebusi, yeye atakuwa mkuu na jemadari. Naye wa kwanza aliyepanda ni Yoabu mwana wa Seruya, naye akawa mkuu. 1 Mambo ya Nyakati 11:6

David said, Whoever strikes the Jebusites first shall be chief and captain. Joab the son of Zeruiah went up first, and was made chief.

Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo huuita mji wa Daudi. 1 Mambo ya Nyakati 11:7

David lived in the stronghold; therefore they called it the city of David.

Akaujenga huo mji pande zote, toka Milo na kuuzunguka; naye Yoabu akautengeneza mji uliosalia. 1 Mambo ya Nyakati 11:8

He built the city round about, from Millo even round about; and Joab repaired the rest of the city.

Naye Daudi akaendelea, akazidi kuwa mkuu; kwa maana Bwana wa majeshi alikuwa pamoja naye. 1 Mambo ya Nyakati 11:9

David grew greater and greater; for Yahweh of Hosts was with him.

Basi hawa ndio wakuu wa mashujaa aliokuwa nao Daudi, waliojitia nguvu pamoja naye katika ufalme wake, pamoja na Israeli wote, ili kumfanya awe mfalme, sawasawa na neno la Bwana alilonena juu ya Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 11:10

Now these are the chief of the mighty men whom David had, who shown themselves strong with him in his kingdom, together with all Israel, to make him king, according to the word of Yahweh concerning Israel.

Na hii ndiyo hesabu ya hao mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu, Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua pamoja. 1 Mambo ya Nyakati 11:11

This is the number of the mighty men whom David had: Jashobeam, the son of a Hachmonite, the chief of the thirty; he lifted up his spear against three hundred and killed them at one time.

Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. 1 Mambo ya Nyakati 11:12

After him was Eleazar the son of Dodo, the Ahohite, who was one of the three mighty men.

Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pasdamimu; ndiko Wafilisti walikokusanyika vitani, palipokuwa na konde limejaa shayiri ;na hao watu wakakimbia mbele ya wafilisti. 1 Mambo ya Nyakati 11:13

He was with David at Pasdammim, and there the Philistines were gathered together to battle, where was a plot of ground full of barley; and the people fled from before the Philistines.

Ndipo hao wakasimama katikati ya konde lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu. 1 Mambo ya Nyakati 11:14

They stood in the midst of the plot, and defended it, and killed the Philistines; and Yahweh saved them by a great victory.

Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hata pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai. 1 Mambo ya Nyakati 11:15

Three of the thirty chief men went down to the rock to David, into the cave of Adullam; and the host of the Philistines were encamped in the valley of Rephaim.

Na Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na walinzi wa Wafilisti wakati ule walikuwa huko Bethlehemu. 1 Mambo ya Nyakati 11:16

David was then in the stronghold, and the garrison of the Philistines was then in Bethlehem.

Naye Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! 1 Mambo ya Nyakati 11:17

David longed, and said, Oh that one would give me water to drink of the well of Bethlehem, which is by the gate!

Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana; 1 Mambo ya Nyakati 11:18

The three broke through the host of the Philistines, and drew water out of the well of Bethlehem, that was by the gate, and took it, and brought it to David: but David would not drink of it, but poured it out to Yahweh,

akasema, Mungu wangu apishe mbali, nisifanye hivi; je! Ninywe damu ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Maana kwa hatari ya nafsi zao wameyaleta. Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu. 1 Mambo ya Nyakati 11:19

and said, My God forbid it me, that I should do this: shall I drink the blood of these men who have put their lives in jeopardy? for with [the jeopardy of] their lives they brought it. Therefore he would not drink it. These things did the three mighty men.

Tena Abishai, nduguye Yoabu, alikuwa mkuu wa wale watatu; kwa kuwa aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua; akawa na jina kati ya wale watatu. 1 Mambo ya Nyakati 11:20

Abishai, the brother of Joab, he was chief of the three; for he lifted up his spear against three hundred and killed them, and had a name among the three.

Katika wale watatu yeye alikuwa mwenye heshima kuliko hao wawili, akawa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. 1 Mambo ya Nyakati 11:21

Of the three, he was more honorable than the two, and was made their captain: however he didn't attain to the [first] three.

Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu; pia akashuka ,akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theruji. 1 Mambo ya Nyakati 11:22

Benaiah the son of Jehoiada, the son of a valiant man of Kabzeel, who had done mighty deeds, he killed the two [sons of] Ariel of Moab: he went down also and killed a lion in the midst of a pit in time of snow.

Huyo akamwua Mmisri, mtu mrefu sana, aliyekuwa wa dhiraa tano urefu wake; na yule Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi; lakini yeye akamshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. 1 Mambo ya Nyakati 11:23

He killed an Egyptian, a man of great stature, five cubits high; and in the Egyptian's hand was a spear like a weaver's beam; and he went down to him with a staff, and plucked the spear out of the Egyptian's hand, and killed him with his own spear.

Mambo hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. 1 Mambo ya Nyakati 11:24

These things did Benaiah the son of Jehoiada, and had a name among the three mighty men.

Tazama, alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu; naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake. 1 Mambo ya Nyakati 11:25

Behold, he was more honorable than the thirty, but he didn't attain to the [first] three: and David set him over his guard.

Tena hawa ndio mashujaa wa majeshi ya askari; Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethlehemu; 1 Mambo ya Nyakati 11:26

Also the mighty men of the armies: Asahel the brother of Joab, Elhanan the son of Dodo of Bethlehem,

Shama Mharodi, Helesi Mpeloni; 1 Mambo ya Nyakati 11:27

Shammoth the Harorite, Helez the Pelonite,

Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abiezeri Mwanathothi; 1 Mambo ya Nyakati 11:28

Ira the son of Ikkesh the Tekoite, Abiezer the Anathothite,

Sibekai Mhushathi, Salmoni Mwahohi; 1 Mambo ya Nyakati 11:29

Sibbecai the Hushathite, Ilai the Ahohite,

Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathi; 1 Mambo ya Nyakati 11:30

Maharai the Netophathite, Heled the son of Baanah the Netophathite,

Itai mwana wa Ribai wa Gibea wa wana wa Benyamini, Benaya Mpirathoni; 1 Mambo ya Nyakati 11:31

Ithai the son of Ribai of Gibeah of the children of Benjamin, Benaiah the Pirathonite,

Hurai wa vijito vya Gaashi, Abieli Mwaibathi; 1 Mambo ya Nyakati 11:32

Hurai of the brooks of Gaash, Abiel the Arbathite,

Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni; 1 Mambo ya Nyakati 11:33

Azmaveth the Baharumite, Eliahba the Shaalbonite,

wana wa Yasheni Mgiloni, Yonathani mwana wa Shama Mharari; 1 Mambo ya Nyakati 11:34

the sons of Hashem the Gizonite, Jonathan the son of Shagee the Hararite,

Ahiamu mwana wa Sharari Mharari, Elifeleti mwana wa Ahasbai; Heferi 1 Mambo ya Nyakati 11:35

Ahiam the son of Sacar the Hararite, Eliphal the son of Ur,

Mmaakathi, Ahia Mpeloni; 1 Mambo ya Nyakati 11:36

Hepher the Mecherathite, Ahijah the Pelonite,

Hezro Mkarmeli, Paarai mwana wa Ezbai Mwarki; 1 Mambo ya Nyakati 11:37

Hezro the Carmelite, Naarai the son of Ezbai,

Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri; 1 Mambo ya Nyakati 11:38

Joel the brother of Nathan, Mibhar the son of Hagri,

Seleki Mwamoni, Naharai Mbeorothi, mchukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya; 1 Mambo ya Nyakati 11:39

Zelek the Ammonite, Naharai the Berothite, the armor bearer of Joab the son of Zeruiah,

Ira Mwithri, Garebu Mwithri; 1 Mambo ya Nyakati 11:40

Ira the Ithrite, Gareb the Ithrite,

Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai; 1 Mambo ya Nyakati 11:41

Uriah the Hittite, Zabad the son of Ahlai,

Adina mwana wa Shiza Mreubeni, mkuu wa Wareubeni, na thelathini pamoja naye; 1 Mambo ya Nyakati 11:42

Adina the son of Shiza the Reubenite, a chief of the Reubenites, and thirty with him,

Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithni; 1 Mambo ya Nyakati 11:43

Hanan the son of Maacah, and Joshaphat the Mithnite,

Uzia Mwashterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri; 1 Mambo ya Nyakati 11:44

Uzzia the Ashterathite, Shama and Jeiel the sons of Hotham the Aroerite,

Yediaeli mwana wa Shimri, na Yoha nduguye, Muzi; 1 Mambo ya Nyakati 11:45

Jediael the son of Shimri, and Joha his brother, the Tizite,

Elieli Mmahawi, na Yeribai, na Yoshavia, wana wa Elnaamu, na Ithma Mmoabi; 1 Mambo ya Nyakati 11:46

Eliel the Mahavite, and Jeribai, and Joshaviah, the sons of Elnaam, and Ithmah the Moabite,

Elieli, na Obedi, na Yaasieli Mmesobai.

1 Mambo ya Nyakati 11:47

Eliel, and Obed, and Jaasiel the Mezobaite.