1 Mambo ya Nyakati 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 10 (Swahili) 1st Chronicles 10 (English)

Basi Wafilisti wakapigana juu ya Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima Gilboa. 1 Mambo ya Nyakati 10:1

Now the Philistines fought against Israel: and the men of Israel fled from before the Philistines, and fell down slain on Mount Gilboa.

Nao Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe; Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli. 1 Mambo ya Nyakati 10:2

The Philistines followed hard after Saul and after his sons; and the Philistines killed Jonathan, and Abinadab, and Malchishua, the sons of Saul.

Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde. 1 Mambo ya Nyakati 10:3

The battle went sore against Saul, and the archers overtook him; and he was distressed by reason of the archers.

Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia. 1 Mambo ya Nyakati 10:4

Then said Saul to his armor-bearer, Draw your sword, and thrust me through therewith, lest these uncircumcised come and abuse me. But his armor-bearer would not; for he was sore afraid. Therefore Saul took his sword, and fell on it.

Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa. 1 Mambo ya Nyakati 10:5

When his armor-bearer saw that Saul was dead, he likewise fell on his sword, and died.

Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu; na nyumba yake yote wakafa pamoja. 1 Mambo ya Nyakati 10:6

So Saul died, and his three sons; and all his house died together.

Kisha watu wote wa Israeli, waliokuwa huko bondeni, walipoona ya kuwa wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo. 1 Mambo ya Nyakati 10:7

When all the men of Israel who were in the valley saw that they fled, and that Saul and his sons were dead, they forsook their cities, and fled; and the Philistines came and lived in them.

Hata ikawa siku ya pili yake Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara hao waliouawa, walimwona Sauli na wanawe wameanguka juu ya mlima Gilboa. 1 Mambo ya Nyakati 10:8

It happened on the next day, when the Philistines came to strip the slain, that they found Saul and his sons fallen on Mount Gilboa.

Wakamvua mavazi, wakamtwalia kichwa, na silaha zake, kisha wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari kwa sanamu zao, na kwa watu. 1 Mambo ya Nyakati 10:9

They stripped him, and took his head, and his armor, and sent into the land of the Philistines round about, to carry the news to their idols, and to the people.

Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa miungu yao, wakakikaza kichwa chake nyumbani mwa Dagoni. 1 Mambo ya Nyakati 10:10

They put his armor in the house of their gods, and fastened his head in the house of Dagon.

Na watu wote wa Yabesh-gileadi waliposikia hayo yote Wafilisti waliyomtenda Sauli, 1 Mambo ya Nyakati 10:11

When all Jabesh Gilead heard all that the Philistines had done to Saul,

wakainuka mashujaa wote, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi, wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga muda wa siku saba. 1 Mambo ya Nyakati 10:12

all the valiant men arose, and took away the body of Saul, and the bodies of his sons, and brought them to Jabesh, and buried their bones under the oak in Jabesh, and fasted seven days.

Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, 1 Mambo ya Nyakati 10:13

So Saul died for his trespass which he committed against Yahweh, because of the word of Yahweh, which he didn't keep; and also because he asked counsel of one who had a familiar spirit, to inquire [thereby],

asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese. 1 Mambo ya Nyakati 10:14

and didn't inquire of Yahweh: therefore he killed him, and turned the kingdom to David the son of Jesse.